Rais Samia kuhutubia bunge Zambia

Rais Samia

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kulihutubia Bunge la Zambia kuhusu misingi ya uhusiano wa Tanzania na taifa hilo.

Kiongozi huyo ametaja miongoni mwa miradi mikubwa ya maendeleo inayohusianisha mataifa hayo ni Reli ya Tazara, bomba la mafuta la Tazama na barabara ya Tanzam ‘The Tanzam Highway’.

Kupitia mtandao wake wa X, Rais Samia ameeleza katika ziara hiyo pia watajadili mwelekeo wa miradi hiyo mikubwa na muhimu, uendeshaji wake na njia za kuiongezea tija zaidi.

Rais Samia yuko nchini Zambia kwa ziara ya kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 59 ya uhuru.

“Leo Zambia ikiwa inatimiza miaka 59 ya uhuru nimepata fursa kutembelea mnara wa mashujaa wapigania uhuru jijini Lusaka, kuweka shada la maua na tafakari fupi kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa nchi hii, hayati mzee Kenneth Kaunda,”ameandika Rais Samia.

Advertisement
3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *