Kwa mujibu wa tetesi za usajili Klabu ya Real Madrid ina majuto makubwa kuhusu kumsajili Kylian Mbappé majira haya ya kiangazi na wamebaki wakiwa wamevunjika moyo kutokana na kiwango chake cha mchezo.
Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, alikuwa mtu pekee aliyetaka kumsajili mfaransa huyo. (Romain Molina)
Barcelona na Bayern Munich zote mbili zimejiunga katika mbio za kumsajili beki wa kulia wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold. (Fichajes – Spain)
Licha ya uvumi wa kurejea Manchester City, Chelsea haitafikiria ofa za kumuuza kiungo nyota, Cole Palmer. (Football Insider)
SOMA: Mbappe, Madrid ngoma inogile
Kipengele cha kumwachia cha beki wa kati wa RB Leipzig, Castello Lukeba kitashuka kutoka pauni milioni 75 hadi 54.2 majira ya kiangazi 2026.
Chelsea, Real Madrid na Aston Villa zote hizo zimehusishwa kutaka kumsajili mfaransa huyo. (Sky Sports Germany)
Newcastle United ipo tayari kuanza tena kufuatilia saini ya beki wa kati wa Crystal Palace, Marc Guehi kwa kuwasilisha ombi la pauni milioni 80 Januari, 2025. (TEAMtalk)
Tottenham Hotspur imeungana na Liverpool katika mbio za kumsajili beki wa kati wa Bayer Leverkusen, Jonathan Tah, ambaye mkataba wake unamalizika majira yajayo ya kiangazi. (Fichajes – Spain)