Samia atoa neno michango shuleni

ZANZIBAR; RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi kuwa tayari kuchangia kiasi kidogo kinachohitajika kuwawezesha wanafunzi kukamilisha mahitaji ya kimasomo kwa sababu seri kali imebeba sehemu kubwa ya gharama za elimu kwa watoto.
Alisema hayo jana akiz indua Shule ya Sekondari ya Bumbwini Misufini iliyoko Kaskazini B, Zanzibar. Alisema ni lazima wazazi watumie fursa ya uwekezaji mkubwa wa serikali kwenye elimu kupeleka watoto wapate elimu kwani ndiyo malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Samia alibadilisha jina la shule hiyo na kuitwa Shule ya Sekondari ya Balozi Seif Bumbwini Misufini akisema kiongozi huyo hajawahi kutajwa katika miradi mbalimbali licha ya kutumikia taifa kwa mafanikio makubwa.
Aidha, Rais Samia alisema uwekezaji katika elimu ni maono ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kusomesha watoto wawe wataalamu na si wasomi kwani kuwa mtaalamu kuna faida kwa nchi lakini kuwa msomi kunaweza kusiwe na faida yoyote kwa taifa.
“Pamoja na kwamba gharama kubwa ikiwa wizara haitajipanga kwa ajili ya kufanya ukarabati kutokana na upungufu utakaojitokeza baadaye. elimu ni bure, serikali tuna beba mzigo wetu, lakini kile kidogo wazazi tunachoomba mtusaidie, tusaidieni.
“Tuna mtindo wa kusema, labda wameambiwa kuna safari fulani ya shule kila mtoto achangie, anasema mie sina pesa si ndio elimu bure, mie sina, hapana,” alisema Rais Samia.
Aliongeza kuwa lengo ni kuandaa wataalamu wenye ujuzi ili kuwaandaa vijana wawe wanafaa kwenye soko la ajira hasa wakati huu am bao uwekezaji unaongezeka Tanzania katika maeneo mbalimbali kama utalii, vi wanda, kilimo, afya na elimu.
Alisema kuna vikwazo mbalimbali vinavyotokana na mila na desturi hali inayo sababisha watoto kuzuiwa kwenda katika shule na vyuo kupata utaalamu unaoweza kuwafanya wawe na maisha bora.
“Kuna changamoto au vizuizi vinavyotokana na mila, mtoto anaulizwa unakwenda wapi, anajibu hoteli, mimi kama mama niliyekuzaa huko hapana, kuna ulevi huko. Lakini ajira za kule sio Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zan zibar, Lela Mohamed Mussa alisema Serikali ya Zanzibar imeleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu katika miundombinu, vifaa na walimu, hali iliyosababisha ufaulu wa watoto kupanda,” alisema Rais.
Alisema kutokana na uwekezaji huo, wanafunzi wa Zanzibar wanapata elimu bora katika mazingira bora. Alisema katika kipindi cha miaka minne, serikali imejenga maghorofa 35 na kubainisha kuwa lengo la serikali ni kuingiza awamu moja badala ya mbili.
Aliongeza kuwa shule hiyo imejengwa na Kampuni ya Simba Developers kwa gharama ya Sh bilioni 6.1 ikiwa na ghorofa tatu na madarasa 40 na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,800.
Alisema watoto lazima wapewe fursa kamili ya kupata elimu kwa sababu ndio wakati wao na Mungu aliiwezesha serikali kufanya uwekezaji huo kwa sababu anajua kuwa kuna watoto wanataka watumie matunda hayo kutoka kwa serikali yao.
Sambamba na hilo, Rais Samia aliwataka viongozi wa maeneo hayo, walimu na wanafunzi kutunza shule na miundombinu yake hiyo ili kuishi kwa muda mrefu na kusaidia watoto wengi kwa vizazi vingi vijavyo.
“Nakumbuka niliwahi kutoa wazo la kuanzisha mfuko wa ukarabati, sasa kama ule mfuko upo naomba shule hizi zibakie hivi zilivyo. Baada ya miaka miwili rangi ikichuja wapaka rangi waje wazitizame na kwa walimu vile vilivyomo ndani ni vya gharama, mnapoenda kuvitu mia mvitunze,” aliongeza Rais Samia.