MFUKO wa Fedha wa SELF uliopo chini ya Wizara ya Fedha umewataka Watanzania kujitokeza viwanja vya Bombadia mkoani Singida Ili kufahamu fursa za uwekezaji za kifedha chini ya mfuko huo.
SOMA: Wananchi Mtwara watakiwa kuchangamkia fursa
Wito huo umetolewa na Linda Mshana ambaye ni Meneja Masoko na Uhamasishaji wa mfuko huo akiwa kwenye maonesho ya saba ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Programu hiyo inahusisha Kanda ya Kati mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Tabora, Manyara Dar-es-Salaam na wenyeji Singida yanayoendelea viwanja vya Bombadia Singida.