Serikali kuongeza nguvu uwekezaji, sekta muhimu

ZANZIBAR: SERIKALI imesema imeweka kipaumbele kwa kuongeza uwekezaji katika elimu, afya, na huduma nyingine za kijamii pamoja na kilimo kinachozingatia hali ya hewa na mazingira.

Hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi akimwakilisha Rais, Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Tathmini ya muda wa kati wa mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaofanyika hoteli ya Golden Tulip uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharib leo Desemba 6, 2023.

Aidha Rais Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Advertisement

Amesema, falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan inayohusu mambo manne ya msingi ya kuzingatiwa ambayo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na ujenzi mpya.

Rais Mwinyi amesema kuwa uchumi wa Zanzibar unanufaika na utalii wa kitamaduni ikiwemo Mji Mkongwe ambao ni eneo la urithi wa dunia.

Amesema Zanzibar ilipata msaada kutoka IDA fedha za kigeni dola za kimarekani milioni 93 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mijini na kuhifadhi mazingira ya urithi wa kitamaduni.

Rais Mwinyi ametolea mfano wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi (COP28) huko Dubai, Rais Dk.

Samia amejitolea kutetea ajenda ya kusaidia kupunguza nishati mimea ambayo huathiri mazingira alipoongoza uzinduzi wa mradi wa Nishati safi ya kupikia itakayowasaidia Wanawake Barani Afrika (AWCCSP).

1 comments

Comments are closed.