Serikali yatoa Sh bil 4 ujenzi wa wodi binafsi Muhimbili

DAR ES SALAAM: SERIKALI imetoa kiasi cha Sh bilioni 4 kuendeleza ujenzi wa jengo la gharofa nne la wodi ya binafsi inayogharimu kiasi cha Sh bilioni 21 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumza leo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi ilipotembelea hospitali hiyo, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Dk Florence Samizi amesema hatua hiyo ni kuhakikisha miradi yote iliyokwama inaendelezwa kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagiza.

“Jengo la huduma binafsi lilisimama kwa muda mrefu na maelekezo la Rais miradi iliyokwama imalizike kabla ya kuanza miradi mingine tayari wizara imeshatoa fedha kumaliza jengo hilo litakuwa na ghorofa nne litajengwa kwa bilioni 21 miradi iliyokwama itakamilishwa,”ameeleza.
Aidha amesema serikali inakwenda kujenga Muhimbili mpya ili kutumia eneo hilo vizuri kwa kujenga ghorofa itakalogharimu kiasi cha Sh trilioni 1.3.

“Jengo hilo linatarajiwa kuchukua miaka saba kuanzia mwaka huu mpaka 2032 na huduma zote za Muhimbili zitawekwa sehemu moja tutakuwa na jengo kubwa la pamoja na tutafanya matumizi bora.
Dk Samizi amesema ujenzi wa Muhimbili mpya hautaathiri utoaji wa huduma zilizopo kwani zitatolewa kama kawaida na baada ya kumaliza majengo hayo watapata ithibati ya kimataifa na Utalii wa matibabu utakua .
Amesema moja ya changamoto iliyopo ni uhaba wa watumishi na wananchi wanaona kuwa wanakaa mda mrefu jambo ambalo limetekelezwa na litaendelea kutekelezawa.
“Lakini miwakubushe kuwa ahadi ya Rais Samia ni kuongeza watumishi hadi sasa nitoe taarifa rasmi kwamba watumishi wa afya 5000 wamekwisha kuajiri watumishi 250 wanaendelea kufanya kazi na Rais ameahidi kuendelea kutangaza kuongeza watumishi kila wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Afya na Masuala ya Ukimwi Dk Johhanes Lukumay amesema hospitali hiyo inahuduma nyungi za kibingwa na kuwataka wananchi kutumiahuduma hizo ipasavyo.
“Wananchi wamekiri huduma ni nzuri na wasiokuwa na uwezo wanapata msamaha wa matibabu kuna mitambo ya kisasa hospitali ina vyumba vya upasuaji 18 na wanakarabati kwa awamu kuna ya akinamama na watoto zitakuwa za kisasa zitagharimu Sh bilioni 1.
Ameongeza “Wamefanya ukarabati katika wodi ya Kibasila,jengo la bima na hospitali inafanya tafiti kubwa za afya sasa inafanya utafiti wa dawa ya kuzuia damu kutoka kwa kinamama waliojifungua.
Ameiomba wizara ya afya kuona namna fedha zinapatikana ili miradi ikamilike.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com