Simba kwenda Misri dhidi ya Tai wa kijani

QATAR: MWAKILISHI pekee Tanzania wa michuano ya Kimataifa, Simba itamenyana na Al Masry hatua ya robo fainali Β ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba wataanzania ugenini nchini Misri dhidi ya Al Masry ( Tai wa Kijani) mchezo utakaochezwa kati ya April 1 au 2 na 8 /9 watarudiana katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
SOMA ZAIDI: Usiseme Simba! Sema mwakilishi wetu
Wekundu hao wa Msimbazi wakifanikiwa kuvuka hatua ya hiyo wanaenda kucheza nusu fainali kati Β mshindi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini Β dhidi ya Zamalek ya Misri.
Simba imefuzu Β hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika ikimaliza kinara wa kundi A, kwa kuvuna alama 13 mbele ya CS Constantine ya Algeria iliyomaliza nafasi ya pili alama 12.



