Soko Kariakoo lazidi kunoga

UONGOZI wa Soko Kuu la Kariakoo umesema takribani asilimia 70 ya wafanyabiashara waliopangiwa vizimba na maduka katika soko jipya tayari wameanza kufanya biashara zao. Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ashraph Abdulkarim, amesema wafanyabiashara wote 1,520 waliokuwa wakifanya biashara katika soko la zamani lililoungua wamepatiwa nafasi katika soko jipya.

Soko hilo lilijengwa upya kwa gharama ya Sh bilioni 28 baada ya kuungua Julai 10, 2021 na kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Februari 8 mwaka huu. Abdulkarim amesema asilimia 80 ya maeneo ya biashara katika soko hilo yametengwa kwa wafanyabiashara waliokuwa katika soko la zamani, huku asilimia 20 iliyobaki ikitangazwa ili kupata wapangaji wapya.

Ameeleza kuwa kati ya wafanyabiashara 1,900 waliokuwa wakifanya biashara awali, wafanyabiashara 1,520 walirudi na kupewa nafasi katika soko jipya, huku nafasi zilizobaki zikitarajiwa kutolewa kupitia mnada. Amesema utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais Samia wakati wa uzinduzi wa soko hilo umefikia zaidi ya asilimia 95. Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kanzidata ya wafanyabiashara na matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato.

Pia ameeleza kuwa hatua zimechukuliwa kuzuia viongozi kuhodhi vizimba kwa kuwa nafasi zote zilitangazwa rasmi na kila mfanyabiashara alikuwa na fursa sawa ya kupata au kukosa.Kwa mujibu wa Abdulkarim, soko hilo lina miundombinu ya kisasa ikiwemo maegesho ya magari yanayoweza kuchukua magari 400 kwa wakati mmoja na zaidi ya magari 900 kwa siku kwa gharama ya Sh 1,000 kwa saa.

Amesema pia kuna kamera zaidi ya 160 za ulinzi ndani ya jengo la soko na askari wamewekwa katika maeneo ya lifti ili kuwasaidia wafanyabiashara na wateja wanaohitaji maelekezo. Aidha, taasisi mbalimbali zimefungua ofisi ndani ya soko hilo ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA). Pia kuna eneo maalumu kwa huduma za uwakala wa fedha.

Abdulkarim amesema mfumo mpya wa malipo unatumia mfumo wa serikali unaoitwa MUSE, ambapo malipo yote yanafanyika kwa njia ya kielektroniki badala ya fedha taslimu kama ilivyokuwa zamani. Ameongeza kuwa serikali imepunguza kodi ya pango kwa wafanyabiashara wa soko hilo kwa kati ya asilimia 10 hadi 17 kulingana na ukubwa wa eneo na aina ya biashara.

Kwa mfano, mfanyabiashara aliyekuwa analipa Sh 120,000 kwa mwezi sasa atalipa karibu Sh 100,000, huku aliyekuwa analipa Sh 100,000 akitarajiwa kulipa karibu Sh 80,000 baada ya punguzo. Pamoja na punguzo hilo, Rais Samia pia alitoa msamaha wa kodi ya pango kwa mwezi mmoja ili kuwasaidia wafanyabiashara kuanza biashara zao katika soko jipya kwa urahisi. SOMA: Kariakoo yatangaza msamaha wa kodi miezi miwili

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button