TAKUKURU kuchunguza miradi ya bil 34/ Tanga

Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa TAKUKURU mkoa wa Tanga, Frank Mapunda.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imeanza uchunguzi wa miradi 79 yenye thamani ya sh Bil 34.5 iliyobainika kuwa na mapungufu katika sekta mbalimbali sambamba na uliyokuwa na mapungufu wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024.

Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa TAKUKURU mkoani humo Frank Mapunda amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024.

SOMA: Mwenge kukagua miradi 87 Tanga

Advertisement

Amesema kuwa miongoni mwa miradi hiyo miradi minne imebainika kuwa na mapungufu kadhaa yaliyopelekea kuanzisha kwa uchunguzi ambapo ameitaja hiyo kuwa ipo katika sekta za Elimu, Barabara, Maji na Afya.

Aliitaja miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya Msingi Kisinga wenye thamani ya Sh.Milioni 50 katika Halmashauri ya Lushoto, Ujenzi wa Zahanati ya Milingano wenye thamani ya shs Milioni 553.

Mapunda ametaja miradi miengine kuwa ni upanuzi wa kituo cha Aya Mgwashi wenye thamani ya shs Milioni 500 na mradi wa zahanati ya Maalie wenye thamani ya Shs Milioni 50..