WAKULIMA wa korosho Wilaya ya Tandahimba na Newala mkoani Mtwara kwa mara ya kwanza wameuza korosho ghafi kwa bei ya juu ya Sh 4,120 na bei ya chini Sh 4035 katika msimu wa kilimo mwaka 2024/2025.
Mnada huo ni kwanza kwa msimu huo wa mwaka ambapo tani 3,857 zimeuzwa kwenye mnada huo uliyofanyika Halmashauri ya Mji Newala mkoani Mtwara chini ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU) mkoani humo kupitia Mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania wa TMX.
Mkulima kutoka kijiji cha Mwangaza wilayani Tandahimba, Rukia Silimu amesema wamepokea kwa furaha kubwa kupanda kwa bei hiyo kwasababu haijawahi kutokea Kwa miaka kadhaa iliyopita.
“Katika kipindi cha miaka mitatu au minne wakulima tulikata tamaa lakini kwa mnada huu tumefuhai sana, na hii ni kwasababu tulipata pembejeo za kutosha uzalishaji umekuwa mzuri sana,”Rukia.
Mkulima kutoka Chama cha Msingi cha Nanguruwe kwenye Halmashauri ya Mji Newala, Sharifu Linjenje “Wakulima tulikuwa na shauku kubwa kujua bei katika mnada huu wa kwanza lakini tumejione na tumefurahi sana, tunaishukuru sana serikali yetu,”
SOMA: Wakulima wa korosho kuelimishwa kuhusu mapato
Mwenyekiti wa Chama Kikuu hicho, Karim Chipola ameishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza jitihada kubwa za kuwapatia wakulima pembejeo bure na kufanya bei kuwa mzuri katika msimu huo hali ambayo haijawahi kutokea.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred amesema mnada huo yameshindana na makampuni 37 ambapo kati hayo, korosho zote zilizouzwa kupitia mnada huo zimenunuliwa na makampuni 10 tu na mengine 27 hayajapata korosho.
Amesema bei hizo zimetikana na uhitaji mkubwa wa korosho karanga kwenye soko la dunia na kuwasisitiza wadau wote waliyoko kwenye mnyororo huo mzima wa thamani katika tasnia hiyo wajitahidi kusimamia ubora.
Mrajisi Msaidizi mkoani humo, Grace Masambaji amesema bei hiyo mzuri imetokana na vile walivyozingatia ubora kwani korosho zao ni safi kutoka kwa mkulima mpaka kufika kwenye ghala kuu.
Mkuu wa Wilaya ya Newala mkoani humo, Rajabu Kundya amesema wanaendelea kuangalia ubora wa korosho zenyewe kutoka mikononi mwa Wakulima kuhakikisha waaondoa unyevu kwenda katika vyamna vya msingi ambavyo navyo walivipa jukumu la kuhakikisha kwamba wanapokea korosho zenye ubira na zenye wa kiwango kinachohitajika.
Akizungumza wakati wa mnada huo, Mkuu wa Mkoa wa Kanali Patrick Sawala wote wanafahamu, ili waweze kuuza korosho zao vizuri kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa ahakikishe korosho zao zinakuwa na ubora wa hali ya juu.