Tanesco yatangaza msamaha wa riba wenye madeni makubwa

WATUMIAJI wa huduma ya umeme wenye madeni makubwa wanaodaiwa na Shirika la Umeme (TANESCO) watapata msamaha wa riba endapo watalipa madeni yao kwa wakati utakaokubalika na shirika hilo.

Katika taarifa yao kwa umma iliyotolewa leo Disemba 11, 2023 kupitia kurugenzi ya mawasiliano, Tanesco imeeleza haitasika kuchukua hatua za kisheria kwa wateja wake wataoshindwa kulipa madeni yao kwa wakati sambamba na kusitishiwa huduma hiyo.

Shirika hilo limeeleza limeanza zoezi la ukusanyaji wa madeni ya ankara za umeme kuanzia Disemba 4, 2023.

Wadaiwa pia wamekumbushwa kulipa madeni hayo ili kuepuka changamoto zitakazojitokeza.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button