‘Tanzania imepiga hatua kubwa utoaji huduma’

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Suleiman Hassan Serera, amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika eneo la utoaji wa huduma, hasa kutokana na ongezeko la watanzania wanaoshiriki moja kwa moja katika uwekezaji na utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Amebainisha hayo wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na Taasisi ya CSW Jijini Dar es Salaam.
SOMA: Tanzania yang’ara biashara duniani
Dk Serera amesema maendeleo hayo yanaonesha namna ambavyo nchi imeendelea kuwaandaa wananchi wake kushiriki kikamilifu katika sekta ya huduma na biashara kwasababu kipimo cha kwanza ni aina ya watu wanaohusika katika uwekezaji na wanaotoa huduma nyingi sasa ni Watanzania wazawa, jambo linaloonesha kuna hatua kubwa katika kuwaandaa.
Ameongeza kuwa ili kuvutia wawekezaji wa nje, ni muhimu kuwa na wananchi walioboreshwa kitaaluma na kiutendaji katika sekta ya huduma.
Amesema imeonekana wazi kuwa watanzania wengi sasa ndio wanaosimamia huduma, kukutana na wateja, na kuendesha shughuli kwa ufanisi mkubwa.
Aidha, Dk Serera ametahadharisha kuwa taasisi au kampuni yoyote isiyotoa huduma bora inahatarisha kupoteza wateja wake, akisema, “Mteja akihudumiwa vibaya, ni rahisi asirudi tena. Hivyo, huduma bora ni msingi wa biashara endelevu.”
Kadhalila, Dk Serera amehimiza taasisi zote, hususan za serikali, kuendelea kuboresha huduma zao, akisema hata wale ambao hawajapata tuzo mwaka huu wamepata fursa ya kujifunza na kuboresha zaidi huduma wanazozitoa kwa wananchi.
Aidha, ameipongeza taasisi ya CSW kwa kuandaa hafla hiyo ambayo ilihusisha utoaji wa zaidi ya tuzo 20 kwa taasisi na kampuni zilizoonyesha ubora wa huduma katika Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa CSW Group, Annelise Nyangusi amesema kuwa katika sekta mbalimbali nchini Tanzania, huduma kwa wateja ni chachu muhimu ya kukuza biashara na kampuni hivyo kama CSW Tanzania, wameona umuhimu wa kutambua na kutunuku kampuni, mashirika na wafanyabiashara wanaofanya vizuri katika utoaji wa huduma kwa wateja, kwa kuzingatia vigezo maalum vinavyoonyesha ubora wa utendaji wao.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com