TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Kriketi imeitandika Lesotho kwa mikimbio 122 mchezo wa hatua ya pili wa makundi wa kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.
Huo ni mchezo wa pili Tanzania inashinda baada ya kwanza kushinda dhidi ya Mali kwa mikimbio 18 na wiketi 10. Wachezaji waliofanya vizuri ni Mohamed aliyeibuka mchezaji Bora wa mechi, akifuatiwa, Amal Rajeevan na Akhil Anil.
SOMA: Tanzania yaanza vyema kriketi U19 Afrika
Matokeo mengine Malawi ilishinda kwa mikimbio 25 dhidi ya Ghana, Cameroon ilishinda kwa wiketi sita,
Ushindi huo unaifanya Tanzania kuongoza kundi lake kwa pointi nne ikifuatiwa na Malawi pointi nne, Ghana pointi mbili, huku Mali pointi moja na Lesotho haina pointi.
SOMA: Mashindano ya kriketi kimataifa kuanza leo
Baada ya kila timu kucheza michezo miwili, michezo itaendelea kesho Jumanne ambapo Ghana itacheza na Lesotho kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.