TARI kutumia teknolojia changamoto za mimea
“TUPO kwa ajili ya kuonyesha aina mbalimbali za teknolojia ambazo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania( TARI), tunaziandaa kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali za kilimo, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk Thomas Bwana anasema.
Dk Bwana ametaja changamoto hizo zinazowakabili wakulima kuwa ni wadudu waharibifu, magonjwa na rutuba ya udongo.
Amesema katika kukabiliana na hali hiyo, TARI ina mbegu mbalimbali zilizofanyiwa utafiti ambazo zinakabiliana na wadudu, magonjwa pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.
“Tuna aina mbalimbali ya mbegu bora za migomba, mbegu za jamii ya mikunde, mpunga,mahindi na korosho.
“Kwa hiyo tunakuwa tunaandaa mbegu bora ambazo zinasaidia katika kukinzana na magonjwa zenye mazai mengi zaidi ili kuongeza tija kwa wakulima,”amesema.
SOMA: TARI yahimiza matumizi ya teknolojia zinazohifadhi mazingira
Teknolojia nyingine alizozitaja Dk Bwana ni ya kitalu mkeka ambayo inasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema teknolojia ya kitalu mkeka mkulima anaweza aka panda mpunga kwa muda mfupi, kwa kuandaa mbegu hata nyumbani, hiyo inasaidia kukimbizana na mvua ambazo zinabadilika basilica.