TARI: Tuna mkungu wa ndizi kilo 110

DAR ES SALAAM; tAASISI ya Utafiti wa Kilimo (TARI), imewaita wadau wa kilimo kujionea teknolojia mbalimbali zilizofanyiwa utafiti ikiwemo ya afya ya udongo, kujua rutuba na uchachu wake.

Mratibu Kitaifa wa Usambazaji Teknolojia na Uhusiano, Mshaghuley Ishika amesema hayo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Soma pia:https://habarileo.co.tz/tari-yahimiza-matumizi-ya-teknolojia-zinazohifadhi-mazingira/

Advertisement

“Tuna teknolojia ya ndizi, tuna ndizi inatisha sana aina ya FHIA 23 ina kilo 110, lakini pia kuna aina ya Taliban 4 ni aina ya ndizi, tumekuja na mkungu wenye kilo 70,” amesema na kuongeza kuwa pia kuna teknolojia mbalimbali za mazao zikiwemo za mbegu lishe, miche ya matunda, pamoja na viungo vya mdalasini, karafuu na vinginevyo.

Amesema wana miche ya minazi na bidhaa zake, kuna ubunifu wametengeneza visheti na kaukau za nazi.

Amesema teknolojia ni nyingi, hivyo wananchi wafike na kujionea katika maonesho hayo.