Temeke kumekucha safari ya Miss Tanzania

DAR ES SALAAM: Warembo 15 wanatarajiwa kushindania taji la Miss Temeke 2026, huku washiriki watano watakaofanya vizuri wakipata nafasi ya kuiwakilisha wilaya hiyo katika mashindano ya Miss Dar es Salaam yanayotarajiwa kufanyika Novemba 12, mwaka huu.

Fainali za Miss Temeke 2026 zimepangwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mbaruku Mwandoro, viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa mashindano hayo, Michael Maurus, amesema Miss Temeke ni  sehemu ya mchakato wa kuelekea mashindano ya Miss Tanzania, ambapo warembo watakaofanya vizuri katika ngazi ya wilaya watapata fursa ya kushiriki Miss Dar es Salaam kabla ya kuendelea na hatua zinazofuata za mashindano hayo.

Amesema maandalizi ya mwaka huu yana umuhimu wa pekee kutokana na matarajio ya Tanzania kuandaa mashindano ya Miss World mwakani, hivyo kuwataka wadau kushirikiana kukuza vipaji na kuwaandaa warembo wenye uwezo wa kuiwakilisha nchi katika majukwaa mbalimbali.

Kwa upande wake, Katibu wa Kamati ya Miss Temeke 2026, Halima Rajabu, amesema warembo hao wanatarajiwa kuanza mazoezi wiki ijayo, huku wakishiriki shughuli za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira na upandaji miti.

Amesema washiriki pia watapatiwa semina maalumu zitakazolenga kuwajengea uwezo kiakili, kimaadili, kiafya na kijamii, ili kuwaandaa kuwa wanawake wanaojiamini, wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya jamii na kuwa viongozi wa baadaye.

Naye Meneja wa Urban Stay Hotel, Chilongawi Julias, amesema hoteli hiyo imeamua kudhamini mashindano hayo kutokana na mchango wake katika kuibua vipaji, kujenga nidhamu na kuimarisha uwezo wa vijana wa kike.

Julias amesisitiza kuwa urembo haupaswi kutazamwa kwa mwonekano wa nje pekee, bali pia unapaswa kuwa jukwaa la kuwawezesha wasichana kujiamini, kukuza vipaji vyao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

  2. ❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa ……………………………………………………………………………….……> https://da.gd/girls66

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button