Thamani miundombinu barabara yafikia tril 40/-

Muonekano kutoka wa angani wa Daraja la Kiyegeya mkoani Morogoro.(Picha na Mfuko wa Barabara )

BODI ya Mfuko wa Barabara (RFB) imesema miundombinu ya barabara ni rasilimali ya umma yenye thamani kubwa zaidi inayokadiriwa kufi kia Sh trilioni 39.5 sawa na asilimia 23 ya Pato la Taifa.

Taarifa ya RFB kwa vyombo vya habari inakadiriwa nchini zaidi ya asilimia 90 na 80 ya abiria na mizigo mtawalia hutumia njia ya barabara kwa ajili ya usafiri na usafishaji.

Katika taarifa hiyo ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, RFB imeeleza serikali imekuwa  ikiimarisha uwezo wa kifedha na kitaasisi ili kuzilinda barabara.

Advertisement

Imeeleza kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia imekuwa ikitenga wastani wa Sh bilioni 900 kila mwaka kuwezesha utekelezaji wa wastani wa miradi 700 ya matengenezo ya barabara za kitaifa na miradi 900 kwa barabara za wilaya na kuimarisha uwezo wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Bodi ya Mfuko wa Barabara.

Taarifa imeeleza hatua za serikali zimewezesha matengenezo ya barabara kufanyika mara kwa mara zaidi ya asilimia 90 za mtandao wa barabara za kitaifa na asilimia 60 za mtandao wa barabara za wilaya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo sehemu kubwa ya mtandao wa barabara unapitika kipindi chote cha mwaka na hali hiyo imeiwezesha Tanzania kuwa moja ya nchi za Afrika zenye mtandao bora wa barabara.

“Kwa kuboresha miundombinu ya barabara, wananchi wamewezeshwa kuzifikia huduma za kijamii na kiuchumi zinazotolewa na serikali kama elimu, afya, masoko, ajira na fursa nyingine za kujipatia kipato.

Bodi ya Mfuko wa Barabara itaendelea kufanya kazi kwa juhudi na umahiri ili kutoa mchango unaotarajiwa kufikia malengo ya serikali,” imeeleza.

Taarifa imeeleza barabara za kitaifa zilizo kwenye hali nzuri zimeongezeka na kufikia wastani wa asilimia 90 kutoka wastani wa asilimia 13 mwaka 2000.

“Aidha, barabara za wilaya zilizo kwenye hali nzuri na wastani, zimeongezeka na kufika asilimia 60 kutoka asilimia 10 mwaka 2000,” imeeleza.

Taarifa ilieleza mtandao wa barabara nchini una jumla ya kilometa 181,602 na kati ya hizo kilometa 37,225.7 ni barabara za kitaifa zinazosimamiwa na Tanroads na kilometa 144,376.5 ni za wilaya chini ya Tarura.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *