TSN, NHIF Kujenga Ushirikiano wa Kidijitali

DAR-ES-SALAAM : MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Asha Dachi, amekutana na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa lengo la kujadili maeneo mapya ya ushirikiano wa kibiashara, hususan katika sekta ya uchapaji na majukwaa ya kidijitali.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za TSN, Tazara jijini Dar es Salaam, ambapo Dachi alieleza kuwa kampuni hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa cha uchapaji, chenye uwezo wa kuchapa nyaraka mbalimbali ikiwemo mabango na vipeperushi.
“Mradi huu upo katika hatua ya asilimia 57 ya ujenzi, huku vifaa vya kisasa vya uchapaji tayari vikiwa vimenunuliwa kwa asilimia 78. Tunawahimiza NHIF kutumia huduma zetu kwa ufanisi zaidi,” alisema Dachi.
Alisisitiza kuwa kwa sasa biashara ya magazeti imebadilika na kuelekea kwenye matumizi ya majukwaa ya kidijitali, hivyo TSN inaendelea kuwekeza kwenye mfumo wa e-paper ili kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.
“Siku hizi dunia imehamia mtandaoni. Tunawakaribisha NHIF kuwa sehemu ya mfumo wetu wa gazeti mtandao kwa ajili ya kusambaza taarifa zao kwa wananchi,” aliongeza.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa NHIF, James Mlowe, alieleza kuwa kupitia ushirikiano huo, NHIF itakuwa na fursa pana ya kuwafikia wananchi wengi zaidi, hasa katika kampeni za kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa bima ya afya.
“Kwa kutumia majukwaa ya TSN, tutapanua wigo wa elimu kwa umma na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mfumo wa afya bora kwa wote,” alisema Mlowe.
Ushirikiano huo unalenga kuongeza ufanisi wa taasisi zote mbili katika kuhudumia jamii na kukuza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma.
SOMA: TSN, Xinhua kuimarisha ushirikiano matumizi AI
Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now, YOU can too with the Home Profit System:
ACT NOW➢ https://Www.Earnapp1.com