Ufunguzi CHAN kufanyika Dar

UFUNGUZI wa mashindano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2025 utafanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza.

Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, mechi ya ufunguzi itafanyika Agosti 2, 2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa na kwamba mechi ya mshindi wa tatu itafanyika Uwanja wa Mandela uliopo Kampala, Uganda, huku fainali ya michuano hiyo ikipangwa kuchezwaUwanja wa Kasarani, Nairobi, Kenya, Agosti 30, 2025.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button