Ulega akoshwa na miradi 81 ya dharura

MOROGORO: Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), akiupongeza kwa usimamizi thabiti wa miradi 81 ya dharura iliyotekelezwa nchini.

Miradi hiyo, iliyohusisha ujenzi wa madaraja na makalvati kupitia mpango maalum wa CERC, imeelezwa kuwa mfano wa mafanikio ya kitaifa katika kukabiliana na changamoto za miundombinu hususan nyakati za mvua na mafuriko.

Akizungumza mkoani Morogoro wakati akifungua Mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS, Ulega amesisitiza kuwa miradi hiyo si tu imekamilika kwa wakati, bali pia imejengwa kwa viwango vya juu vya ubora na Makandarasi wazawa jambo linaloonesha kukua kwa uwezo wa ndani wa kitaalamu.

Waziri Ulega amemshukuru Rais, Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo, akibainisha kuwa uwekezaji huo umeanza kuzaa matunda.

Ameongeza kuwa licha ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini mwaka huu, athari zake zimepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma hali inayochangiwa na ubora wa miundombinu iliyojengwa.

“Miradi hii ya dharura ni alama ya uwezo wa wataalam wetu wa TANROADS katika kusimamia na kutekeleza kazi kwa umahiri mkubwa. Ni mfano hai wa namna tunavyoweza kukabiliana na changamoto za mafuriko nchini”, amesisitiza Ulega.

Katika kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo, Waziri Ulega amewataka viongozi na watumishi wa TANROADS nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu, sambamba na kuzingatia nidhamu kazini.

Amesisitiza umuhimu wa kulinda na kuendeleza misingi iliyoasisiwa na waanzilishi wa Wakala huo kwa lengo la kuijenga Tanzania yenye miundombinu imara.

Aidha, ametoa maelekezo mahsusi ya kuhakikisha matengenezo ya barabara na madaraja yanafanyika kwa wakati ili kupunguza usumbufu kwa wananchi.

Pia, ameelekeza utekelezaji wa mpango wa kupendezesha barabara kwa kupanda miti ya kivuli na matunda takribani 1,000 kwa kila mkoa, pamoja na kuimarisha uwekaji wa taa za barabarani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala ameishukuru Serikali kupita Wizara ya Ujenzi kwa kutoa malipo ya awali Mkandarasi anayejenga barabara ya Bigwa – Kisaki (km 78) kwa kiwango cha lami na kueleza kuwa mradi huo tayari umeanza huku akifafanua kuwa wananchi wa Kinole na Mbingu watakuwa wanufaika wakubwa wa ujenzi wa miundombinu hiyo.

Awali, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, ameeleza kuwa mkutano huo ni jukwaa muhimu unalenga kuimarisha ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maamuzi ya kiutendaji na kupanga mikakati ya maendeleo ya taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, akimwakilisha Katibu Mkuu, Karim Mkorehe amemhakikishia Waziri Ulega kuwa TANROADS itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa, kwa lengo la kuongeza ufanisi wa Taasisi na kuhakikisha wananchi wanapata miundombinu bora, salama na ya kisasa.

Habari Zifananazo

13 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

    1. 고양이분양이라니 너무 설레이는 소식이네요! 동탄 지역의 사람들에게 행복한 가정을 찾아주는 모습이 너무 좋아요. 고양이들은 정말 사랑스럽고 품격 있어서 만나면 누구든 행복해질 것 같아요. 축하드려요! 동탄고양이분양

    2. 포메라니안은 정말 귀엽고 사랑스러운 견종이에요. 그 작은 몸집에 담긴 활기찬 에너지와 애교로운 행동들이 매력적입니다. 또한, 그들은 주인을 매우 애정스럽게 대해주는 충실한 친구이기도 해요. 정말 사랑스러운 반려견이에요! 포메라니안

    3. 말티푸는 귀엽고 사랑스러운 강아지 종류이죠. 그 작고 아름다운 몸매와 사교적인 성격으로 많은 사람들의 마음을 사로잡고 있습니다. 말티푸와 함께하는 것은 행복과 즐거움으로 가득할 것 같아요. 집안에 활기를 불어넣어주는 그 모습은 정말 멋지죠. 말티푸

    4. 저에게는 페르시안 고양이와 스코티쉬 폴드가 가장 매력적으로 보여요. 페르시안 고양이의 우아함과 스코티쉬 폴드의 귀여움에 마음이 끌려요. 고양이종류에도 여러 가지 매력이 있어서 선택하기가 어려워요. 고양이종류

    5. 강아지를 분양받는 건 정말 특별한 경험이에요. 새로운 가족 구성원을 맞이하는 기쁨과 책임감을 느끼게 되죠. 강아지와 함께 하는 일상은 정말 행복하고 따뜻한 시간들이 많아요. 분양 전에 충분한 고민과 준비를 통해 사랑을 가득 전해주는 새로운 가족 구성원을 맞이해보세요. 강아지분양

    6. 비숑은 사랑스러운 외모와 친근한 성격으로 많은 사람들의 사랑을 받는 강아지 종류이죠. 그들의 부드러운 털과 유니크한 모습은 마치 눈을 즐겁게 하는 예술작품 같아요. 비숑과 함께하는 시간은 항상 행복하고 편안하게 보낼 수 있는 특별한 시간이 되죠. 비숑

    7. 시바견은 귀여운 외모와 재미있는 성격으로 많은 사랑을 받고 있는 종이에요. 그들의 똑똑함과 활발함은 주인들에게 큰 기쁨을 주죠. 시바견과 함께하는 시간은 항상 유쾌하고 활기찬 것 같아요. 어디서든 주인을 따라 다니고 즐거움을 나누는 모습이 정말 매력적이에요. 시바견

    8. 그레이하운드는 우아하고 활동적인 개 종족 중 하나로, 그 아름다운 체형과 민첩한 모습에 매료됩니다. 그들은 운동을 좋아하여 산책이나 달리기를 통해 에너지를 소비하는 것을 즐기고, 친근하고 사교적인 성격으로 주인과 가족들에게 끝없이 사랑받는 친구가 되어줍니다. 그레이하운드

    9. 골든리트리버는 정말 사랑스러운 강아지 종류이죠. 그들은 상냥하고 친근하며 똑똑해서 가족들과 함께 지내기에 딱 좋은 반려견이에요. 그들의 활발하고 밝은 에너지는 누구나 환영받는 기분을 만들어주죠. 골든리트리버와 함께하는 시간은 행복이 가득한 특별한 경험이라고 생각해요. 골든리트리버

    10. 브리티쉬숏헤어는 정말 멋진 품종이에요! 그들의 단정한 외모와 사교적인 성격은 매력적이에요. 브리티쉬숏헤어와 함께하는 시간은 항상 즐겁고 편안해요. 어디서나 주목을 받는 그들의 아름다움은 정말 대단하죠. 브리티쉬숏헤어

    11. 비숑프리제는 활기차고 사랑스러운 성격으로 유명한 견종이에요. 그들의 부드러운 털과 귀여운 외모는 많은 사람들의 마음을 사로잡았죠. 활발한 에너지와 사교적인 성격 때문에 가정에서 활약하기에 안성맞춤이죠. 또한 털이 자주 떨어지지 않아 관리도 비교적 쉽답니다. 집안에 활력을 불어넣어주는 비숑프리제와 함께하는 삶은 정말 행복할 것 같아요 비숑프리제

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button