Ushirikiano wahitajika chakula shuleni

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidhi Ameir ametoa wito kwa wadau wa elimu, wazazi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula bora na maji safi wakiwa shuleni ili kuboresha afya zao na kuongeza ufaulu wa kitaaluma.
Akizungumza leo Machi 12, 2026, katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni na Siku ya Kimataifa ya Chakula Shuleni, yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma, Ameir amesema lishe bora kwa wanafunzi ni msingi muhimu wa kujifunza kwa ufanisi.
Amesema wanafunzi hutumia muda mwingi wakiwa shuleni, hivyo upatikanaji wa chakula bora, maji safi pamoja na mazingira salama ya usafi ni muhimu katika kulinda afya zao na kuongeza uwezo wao wa kujifunza. “Kaulimbiu ya mwaka huu inayosema ‘Chakula Bora, Maji Safi Shuleni: Ni Wajibu wa Pamoja’ inatukumbusha kuwa jukumu la kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe bora si la Serikali pekee, bali linahitaji ushiriki wa wadau wote,” alisema Wanu .

Aidha, amezipongeza taasisi na wadau wa maendeleo wanaoshirikiana na Serikali katika kuimarisha mpango wa lishe shuleni, wakiwemo UNICEF, WFP, Children in Crossfire, GAIN Tanzania, Action Against Hunger, pamoja na kampuni ya SANKU, kwa mchango wao katika kufanikisha maadhimisho hayo. Wanu pia amewahimiza wazazi kushirikiana na shule kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma ya chakula shuleni kwa mujibu wa Waraka wa Elimu Na. 3 wa mwaka 2016.
Maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni yalianzishwa mwaka 2016 kufuatia makubaliano ya Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, yakilenga kuhamasisha upatikanaji wa chakula na lishe bora kwa wanafunzi kupitia ushirikiano wa Serikali, mashirika ya kimataifa pamoja na jamii.

Maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni yalianzishwa mwaka 2016 kufuatia makubaliano ya Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, yakilenga kuhamasisha upatikanaji wa chakula na lishe bora kwa wanafunzi kupitia ushirikiano wa Serikali, mashirika ya kimataifa pamoja na jamii. SOMA: Dk Mpango: JKT wezesheni Tanzania kuwa ghala la chakula Afrika




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com