Vijiji 785 vyafikiwa na umeme wa Rea Mtwara

WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) wamekamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vyote 785 katika Mkoa wa Mtwara.

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA) Jones Olotu amesema hayo leo Octoba 28 wakati wa hafla ya uzinduzi wa umeme katika kijiji cha mwisho cha Makome Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Amesema ukamilishaji huo umetokana na mradi mkubwa wa REA III round two ambao ulizinduliwa mwaka 2021 ukilenga kusambaza umeme kwenye vijiji 401 ambavyo havikuwa na umeme.

Advertisement

SOMA: Mabilioni ya REA kukiongezea kilimo thamani

“Wakati tunazindua huo mradi katika mkoa wa Mtwara (REA III round two) mwaka 2021 vijiji 384 tu ndivyo vilikuwa na umeme , na tuliweka wakandarasi wawili na kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa kusambaza umeme kwenye 401 ambavyo vilikuwa vimebaki,” amesema.

Kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaitaka REA kuhakikisha inasambaza umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2025.

“Kwenye upande wa vijiji hatuna deni, na hiyo maana yake kwenye Ilani ya Chama ambayo inatutaka sisi tupeleke umeme kwenye vijiji vyote kabla ya mwaka 2025,” amesema.

Akizungumza mara baada ya kuzindua umeme huo katika kijiji cha mwisho cha Makome, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka wananchi wa mkoa huo kutunza miundombinu wa nishati hiyo ili iweze kuwaletea matokea chanya kwenye uchumi na shughuli nyingine za maendeleo.

SOMA: Umeme kusambazwa vitongoji 134 Ruvuma

1 comments

Comments are closed.