MICHEZO ya Ligi Kuu tano bora barani Ulaya inaendelea leo kwenye viwanja tofauti England, Hispania, Ujerumani, Italia na Ufaransa.
Majogoo Liverpool inaongoza Ligi Kuu England(EPL) ikiwa na pointi 57 baada ya michezo 24 huku Southampton iko mkiani ikiwa na pointi tisa.
Katika LaLiga, Real Madrid ni vinara hadi sasa ikiwa na pointi 50 baada ya michezo 23 wakati Real Valladolid ni mwisho wa msimamo ikiwa na pointi 15.
Miamba ya Bavaria, Ujerumani, Bayern Munich yenye pointi 54 baada ya michezo 21 hadi sasa ndio inaongoza Ligi Kuu ya Bundesliga na klabu inayozibeba timu zote 18 za ligi ni VfL Bochum yenye ponti 11.
Huko Italia baada ya michezo 24 ya Serie A, Napoli ni vinara ikiwa na pointi 55 wakati Monza ni ya mwisho ikikusanya pointi 13.
Katika Ligue 1 ya Ufaransa, Paris Saint-Germain imefikisha pointi 53 baada ya michezo 21 huku Montpellier yenye pointi 15 inajiuliza mwisho wa msimamo wa ligi.
Mitanange inayopigwa leo katika ligi hizo ni kama ifuatavyo:
PREMIER LEAGUE
Leicester City vs Arsenal
Aston Villa vs Ipswich Town
Fulham vs Nottingham Forest
Manchester City vs Newcastle United
Southampton vs Bournemouth
West Ham United vs Brentford
Crystal Palace vs Everton
LALIGA
Leganes vs Deportivo Alaves
Osasuna vs Real Madrid
Atletico Madrid vs Celta Vigo
Villarreal vs Valencia
BUNDESLIGA
St. Paul vs Freiburg
Union Berlin vs Borussia M’gladbach
VfB Stuttgart vs Wolfburg
VfL Bochum vs Borussia Dortmund
Bayern Leverkusen vs Bayern Munich
SERIE A
Atalanta vs Cagliari
Lazio vs Napoli
AC Milan vs Hellas Verona
LIGUE 1
Marseille vs Saint-Etienne
AS Monaco vs Nantes
Toulouse vs Paris Saint-Germain