MACHO na masikio ya wapenda soka duniani leo yataelekea mji mkuu wa Hispania, Madrid kunakofanyika mchezo wa watani wa jadi(Derby) kati ya Real Madrid na Atlético Madrid ikiwa ni Ligi Kuu ya nchi hiyo, LaLiga.
Real Madrid inaongoza LaLiga ikiwa na pointi 48 sawa na Atletico Madrid baada ya michezo 22 lakini Real ina mabao 50 ya kufunga wakati Atletico ina 37.
Real Madrid ni mwenyeji katika ‘Derby’ hiyo kwenye uwanja wa Santiago Bernabéu.
Real inaingia kwenye mchezo huo ikikumbwa na majeruhi eneo ulinzi ambapo Antonio Rudiger, Eder Militao, Dani Carvajal na David Alaba wanatarajiwa kukosekana.
Kwa upande wa Atletico, mchezaji pekee anayetarajiwa kukosekana ni Robin Le Normand, ambaye anatumikia adhabu ya kadi tano za njano.
Mechi nyingine za LaLiga na ligi nyingine tatu bora Ulaya zinazopigwa leo ni kama ifuatavyo:
LALIGA
Celta Vigo vs Real Betis
Athletic Club vs Girona
Las Palmas vs Villarreal
BUNDESLIGA
Borussia Dortmund vs VfB Stuttgart
Freiburg vs FC Heidenheim
Hoffenheim vs Union Berlin
Mainz 05 vs Augsburg
Wolfsburg vs Bayer Leverkusen
Borussia M’gladbach vs Eintracht Frankfurt
SERIE A
Hellas Verona vs Atalanta
Empoli vs AC Milan
Torino vs Genoa
LIGUE 1
Nice vs Lens
Lille vs Le Havre
Saint-Etienne vs Rennes