Wahamiaji 164 wa kisomali warejea kwao

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Somalia, Ahmed Maalam Faqi, ameongoza Kamati ya Wahamiaji wa Kisomali kurejea makwao kupokea vijana 164 wa Kisomali kutoka Libya.

Mpango huo uko chini ya mfumo wa Kurudi kwa Wahamiaji wa Kisomali kwa misingi ya Kibinadamu kwenda kwao, kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya(EU), Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Wakimbizi, pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano.

SOMA: Denmark, Rwanda kushirikiana kuhudumia wahamiaji

Vijana 55 kati yao wamewasili eneo la Hargisa na 109 wamewasili katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za Jamhuri ya Shirikisho la Somalia kushughulikia changamoto za uhamiaji

Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, pamoja na maafisa wakuu wa serikali, imethibitisha kujitolea kwa serikali kulinda raia wa Somalia walioko nje ya nchi na kuwasaidia kurejea nyumbani.

Habari Zifananazo

Back to top button