Waliokosa nafasi kugombea washauriwa kukubali matokeo

DODOMA : WENYEKITI wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA), Wilaya ya Dodoma, Bashiru Omary amewaomba wagombea wa vyama vya siasa katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani ambao wamekatwa na ha- wajapata nafasi ya kuteuliwa kugombea wanatakiwa washirikiane na wagombea walioteuliwa katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.

Wagombea waliokatwa au watakaokatwa na vyama vyao, wanatakiwa kuondoa tofauti zao na kuacha mivutano ya kisiasa, badala yake washirikiane na wagombea walioteuliwa kugombea nafasi hizo katika kuleta maendeleo kwa jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa amewataka wagombea waliokatwa au watakao- katwa na vyama vyao kuacha mivutano isiyo na tija, bali wawe kitu kimoja katika kuleta maendeleo kwa faida ya Watanzania. Aidha, alisema wagombea hao ambao hawakupitishwa na vyama vyao wametakiwa kuvunja makundi ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi, ikiwemo na kulinda amani iliyopo.

Alisema kuendelea kwa mivutano ya kimakundi kunaweza kusababisha mipasuko kwenye vyama na hivyo kusababisha wananchi kutopata maendeleo stahiki. Mwenyekiti huyo pia aliwataka wagombea waliopitishwa na vyama vyao na watakaoshindwa kwenye uchaguzi Oktoba mwaka huu wote washirikiane katika kuwatumikia Watanzania kwa kuwatatulia changamoto zao zinazowakabili, badala ya kutanguliza maslahi yao binafsi.

Aliwataka pia wabunge na madiwani watakao chaguliwa wasitumie nafasi zao kama sehemu ya kuwakandamiza wananchi wanaowapigia kura, bali wakashirikiane katika kufani- kisha mahitaji kama vile ya elimu, afya, barabara, maji na kilimo.

Omary pia aliwakum- busha viongozi ndani ya nyumba za ibada kuendelea kutoa elimu ya ubaya wa kutoa na kupokea rushwa hususani katika kipindi hiki kinachoelekea kwenye uchaguzi mkuu. “Suala la rushwa hata ndani ya vitabu vya dini vinakataza maana tu naelezwa kuwa mtoa rushwa na mpokea rushwa wote hao Mungu amewalaani,” alisema.

Hivyo viongozi ndani ya nyumba za ibada ni muhimu wakawaelimisha waumini kujiepusha na dhambi hiyo inayokatazwa na hata na Mungu mwenyewe. SOMA : Kampeni za Dk Nchimbi zilivyowasha moto wa ushindi Mwanza

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button