SONGWE: Wanafunzi wa shule ya sekondari Wiza iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe, wameiomba serikali kuweka mkakati mashuleni utakaosaidia kuwabaini wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.
Wanafunzi hao wametoa wito huo kwa serikali Oktoba 11, 2023 kufuatia ziara za uelimishaji zinazofanywa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya kutoa elimu maeneo mbalimbali hususani mashuleni na kwenye nyumba za Ibada kuhusiana na dhana ya Ushirikishwaji wa Jamii ambayo msingi wake mkubwa ni kutokomeza vitendo vya uhalifu na wahalifu pamoja na ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Wanafunzi hao wa shule ya Wiza wamesema, ili kutokomeza vitendo hivyo wanaiomba serikali kuweka utaratibu maalum kupitia wataalam wa afya ili waweze kuwabaini wanafunzi wanaojihusisha na uhalifu kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza janga la ongezeko la mmomonyoko wa maadili.