WANAWAKE katika kata ya Vigaeni Manispaa ya Mtwara-Mikindani mkoani Mtwara wametakiwa kupinga vitendo vya ukatili vya aina yoyote kwa watoto na upande wao pia.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mtwara (Juwam) Mariam Chimbwai amesema kutokana na uwepo wa vitendo hivyo wameona ipo haja ya kutoa elimu hiyo ili waweze kubadilika.
Aidha katika utoaji wa mada hiyo wanawake hao wameonesha kuguswa na elimu iliyotolewa kwa sababu itawasaida kupata uelewa mzuri zaidi juu ya vitendo hivyo ambavyo wamekuwa wakiwafanyiwa baadhi ya wanawake.
‘’Leo nimefurahi sana nimeona wanawake wamefurahi kwenye hii mada ya ukatili, wametoa ushuhuda mbalimbali na kupatiwa namba 116 ya kuweza kupiga simu moja kwa moja na kuweza kupata msaada bila kujilikana namba zao za simu zaidi ya yule tu watakaempigia kwa ajili ya kulinda usalama wao,’’amesema Chimbwai.
Amesema elimu hiyo inayotolewa ni kupitia mradi wa Sauti Zetu unaotekelezwa kwa muda wa miezi sita kuanzia Septemba 2024 hadi Februari 2025 katika kata tatu mkoani humo ikiwamo kata hiyo ya Vigaeni, Msangamkuu na Naumbu zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kupitia ufadhili wa Shirika la Women Fund.
SOMA: Vibanda umiza tishio ukatili wa kingono
Katibu Mtendji wa Jukwaa hilo, Judith chitanda amesisitiza elimu hiyo kwa wanawake hao kuwa waache kuficha pale wanapoona uwepo wa vitendo hiyo katika jamii kwa sababu wanaamini vitendo hivyo vipo na vinaendelea kwenye jamii na kutoa mfano kwamba kwa sasa ndoa nyingi zinavunjika kutokana na vitendo vinavyofanywa na wanaume katika ndoa zao.
SOMA: Gwajima: Pato la taifa linateketea kupambana na ukatili
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa hiyo, Godlove Miho ametoa rai wa wanawake hao kuwa kupitia elimu hiyo wakawe mabalozi kwa jamii ili ipate uelewa na kutoa taarifa wanapoona uwepo wa vitendo hivyo kwao na watoto katika maeneo yao na kufanya hivyo itasaidia kuondokana na vitendo hivyo.
Aidha kila penye watoto 10 wa kike watoto watatu wanafanyiwa ukatili, kila penye watoto saba wa kiume mmoja anafanyiwa ukatili na katika wanawake 100 wanawake 20 wanafanyikwa vitendao hivyo.
SOMA: Ushoga, ukatili wa kijinsia jela miaka 30
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Fatuma Dogoa mkazi wa mtaa wa mabatini ‘A’ katika manispaa hiyo amesema: ‘’Elimu ambayo imetolewa naomba iendelee kutolewa ili watu wazidi kuelimika juu vitendo hivi kwasababu matukio mengi yanafanyika lakini watu wanaficha.”