Washauriwa kurudisha kwa jamii

TAASISI, kampuni na mashirika yakumbushwa kurudisha kwa jamii kile wanachokipata kutoka kwa wateja ili kuifikia jamii wenye uhitaji.

Meneja Rasilimali Watu Frolentina Ninnah, kutoka Hoteli ya Dar es Salaam Serena amesema hayo wakati wa kushiriki msimu wa Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa watoto yatima waliojumuika hotelini hapo.

Flolentina amesema bado inahitaji nguvu kubwa kwa taasisi, makampuni na mashirika kuona nafasi ya kusherehekea sikukuu  na watoto yatima ambao wanahitaji faraja zaidi katika jamii.

“Kwa mwaka huu tumeanza kusherehekea na watoto zaidi ya 100 kutoka vituo viwili ni desturi kampuni tumeona kila mwaka turejeshe kwa jamii hasa kwa watoto ambao wanahitaji faraja hasa katika msimu huu Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ambapo tunaamua kurudisha kwa kuigusa jamii.

‘’Tuhakikisha tunajumuika nao katika kula chakula cha pamoja na kuwapa mahitaji mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule na chakula kwa ujumla lakini bado haitoshi kwa sisi peke yake tunaomba na wenzetu waguswe tunachokifanya ili waweze kufanya zaidi ya hiki kwani vituo vipo vingi zaidi”.amesema

Aidha kwa upande wake mkuu wa kituo cha watoto Yatima Malaika Kids , Khadija Said ametoa pongezi kwa uongozi wa hoteli hiyo kwa kuwapa faraja watoto hao wenye uhitaji katika vituo vya kulelea .

 

Habari Zifananazo

Back to top button