WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 01, 2024 anafungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni.
Maonesho hayo pia yanafanyika katika mikoa mingine nchini.
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.”