Yanga vs Azam: ‘Derby’ ya kisasi au rekodi?

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo inashuka dimbani katika mechi ya ‘Derby’ ya Dar es salaam dhidi ya Azam ikishikilia rekodi ya kutopoteza mchezo wala kufungwa bao katika raundi nane.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Yanga inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 24 baada ya michezo nane wakati Azam ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 18 baada ya mechi 9.

Advertisement

SOMA: Yanga kuanza kutetea ubingwa Ligi Kuu leo

Kwa mara ya mwisho Yanga na Azam zilikutana Agosti 11 katika fainali ya Ngao ya Jamii, Yanga ikiibuka bingwa kwa ushindi wa mabao 4-1.

Sambamba na ‘derby’ hiyo leo Singida Black Stars itaikabirisha Coastal Union kwenye uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Singida Black Stars ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22 baada ya michezo 9 wakati Coastal Union ni ya tisa ikiwa na pointi 11 baada ya 10.