MSANII wa Bongo Fleva, Zuhura Othuman ‘Zuchu’ ameuliza swali lake kwa waandaaji wa tuzo za Tanzania Music Awards kuwa wanaangalia kazi wanazofanya wasanii au wanataka kuweka usawa kwa kumfurahisha kila msanii.
Zuchu ameandika kwenye mtandao wake wa Instagram kuwa: “Ni muhimu sana mijadala ya tuzo ikaanza kwa maendeleo ya tasnia Tanzania Music Awards hongereni sana kwa kuendelea kuboresha.
“Lakini inabidi kamati ijibu maswali kadhaa Je mnataka kubalance (kuweka usawa) mezani na kutafuta kumfurahisha kila msanii au mnachotizama ni nini?”ameandika Zuchu.
SOMA: Zuchu afungiwa miezi sita
Hayo yamekuja baada ya ‘Zuchu’ kushinda Mwanamuziki Bora wa Kike na Faustina Mfinanga ‘Nandy’ kushinda Msanii Bora wa Kike hali iliyoibua mijadala mingi mitandaoni kuwepo kwa usawa wa tuzo hizo na kuonekana kama ni tuzo moja.