Samia kuzindua mfuko kuwezesha vijana sekta ubunifu

ARUSHA; WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuzindua rasmi Mfuko wenye jumla ya Sh Bilioni 50 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wanaojihusisha na sekta ya ubunifu nchini.

Akizungumza jijini Arusha Machi 11, 2026, Waziri wa wizara hiyo, Paul Makonda amesema mfuko huo unatarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sekta hizo.

Amewataja wanufaika wa mfuko huo kuwa ni pamoja na watengeneza maudhui mtandaoni (content creators), wasanii, wanamuziki, waigizaji, waandishi wa habari, influencers pamoja na wabunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.

Waziri Makonda amesema awali wizara ilikuwa imepangiwa Shilingi Bilioni 20, lakini baada ya mazungumzo na Benki ya CRDB, kiwango hicho kimeongezwa na kufikia jumla ya Sh Bilioni 50 ili kupanua wigo wa vijana watakaonufaika na mfuko huo.

Ameeleza kuwa, kwa sasa kinachosubiriwa ni tarehe rasmi ya uzinduzi wa mfuko huo, ambapo baada ya uzinduzi fedha hizo zitaanza kutolewa kwa vijana waliopo katika sekta ya habari, sanaa na ubunifu ili kuwawezesha kukuza kazi zao na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Hatua hiyo ni kuwa sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha vijana wanapata fursa za kiuchumi na kutumia vipaji vyao kama chachu ya maendeleo ya Tanzania.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. These mood gummies cbd thc were certainly the amicable of product that works well for a nighttime routine. The flavor was jam-packed, not too lyric, and there wasn’t any quaint hemp-heavy savour hanging wide afterward. They also befitting utterly as slacken gummies because the blanket vibe felt together quiet and easygoing. As anyone browsing nod off gummies, this well-wishing of artefact makes sanity too because it pairs unqualifiedly nicely with a quiet evening, a big, or just slowing things down at the incessantly of the day.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button