Uwekezaji wa serikali wafikia tril 92.3/-

MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema uwekezaji wa serikali ndani na nje ya nchi umeongezeka kwa asilimia saba. Taarifa ya Mchechu imeeleza hadiJuni 30, mwaka huu uwekezaji huo ulifika Sh trilioni 92. 29 kutoka Sh trilioni86.3 mwaka wa fedha 2023/2024.

Imeeleza uwekezaji huo unahusisha mashirika ya umma 255, kampuni 45 ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache na taasisi za kigeni 10 ambazo kwa pamoja zinatengeneza uti wa mgongo wa mapato yasiyo ya kodi ya Tanzania.

Mchechu ameeleza katika kipindi cha miaka mitano, uwekezaji wa ndani umeongezeka kutoka Sh trilioni 67.01 mwaka 2020/2021 hadi Sh trilioni 90.61 mwaka 2024/2025.

SOMA: Waishukuru Serikali mazingira mazuri ya uwekezaji

“Ukuaji huu wa uwekezaji una- onesha maboresho katika utawala wa mashirika ya umma, uhusiano wake na malengo ya maendeleo ya taifa,” amesema Mchechu.

Taarifa ya Msajili wa Hazina ya mwaka ulioishia Juni 30, mwaka huu inaeleza thamani ya uwekezaji wa serikali katika taasisi za nje ulikua kutoka Sh bilioni 722.94 hadi Sh trilioni 1.68.

Mchechu amesema ukuaji huo umetokana na utendaji bora wa mashirika muhimu ya umma na ufanisi katika uendeshaji wa taasisi mbalimbali.

Ametoa mfano Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliorekodi ongezeko la asilimia 29 katika mali halisi, kutoka Sh trilioni 7.2 hadi Sh trilioni 9.3.

Amesema kichocheo kikubwa ni uandikishaji wa wanachama wapya kutoka sekta isiyo rasmi na ujumuishaji na mifumo mingine ya serikali kama Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Mamlaka ya Mapato Tanza- nia (TRA).

Mchechu amesema Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ulionesha ongezeko la asilimia 13 katika mali halisi kutoka Sh trilioni 8.12 hadi Sh trilioni 9.2.

Amesema Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pia iliripoti ongezeko la mali halisi lililokuwa kwa asilimia 82 kutoka Sh trilioni 1.3 hadi Sh trilioni 2.36, ikiwa ni matokeo ya utendaji wa kifedha na usimamizi wa akiba.

Mchechu amesema ongezeko la jumla la uwekezaji wa serikali limechangiwa pia na taarifa za kifedha zilizoboreshwa, ambazo sasa zinaonesha thamani halisi ya hisa na mitaji ya serikali.

“Tumeona pia ongezeko la akiba na faida zilizokusanywa katika mashirika kadhaa, sambamba na kuongezeka kwa faida katika mashirika mengi ya umma,” amesema.

Hata hivyo, kwa baadhi ya mashiri- ka hasa yale yaliyoko kwenye hatua za maendeleo kama kampuni za madini, yalishuhudia kupungua kwa mtaji kutokana na matumizi makubwa ya uwekezaji na kuwa na mapato madogo.

Kwa ujumla, uwekezaji wa serikali unatawaliwa zaidi na mashirika ya- siyo ya kibiashara, ambayo yanabeba asilimia 72 ya uwekezaji wa Sh trilioni 65.44, ikilinganishwa na Sh trilioni 25.17 (asilimia 28) zilizowekezwa katika mashirika ya kibiashara.

Uwekezaji wa nje

Uwekezaji wa serikali katika taasisi 10 za nje ulipanda kwa kasi na kufikia Sh trilioni 1.68 kufikia Juni 30, mwaka huu, sawa na ongezeko la asilimia 98 kutoka Sh bilioni 846.22 mwaka uliopita.

Taarifa ya Ofisi ya Msajili wa Hazina inaonesha ongezeko la asilimia 34 katika mapato yasiyo ya kodi kutoka Sh bilioni 767 mwaka 2023/2024 hadi Sh trilioni 1.03 mwaka 2024/2025.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button