TTCL yajizatiti teknolojia ya kisasa

DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema linaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa na kuboresha mifumo yao kwa ajili ya kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma bora ya intaneti ya kasi kupitia huduma ya Faiba mlangoni kwako.
Mkurugenzi wa Sheria wa TTCL,Anita Moshi wakati akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TTCL,Moremi Marwa alisema hayo Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa wiki ya huduma kwa mteja.
Alisema huduma ya faiba mlangoni kwako inalenga kupeleka huduma ya intaneti ya kasi ya kufaiba moja kwa moja kwenye nyumba za wakazi wa eneo husika.
Alieleza kuwa Faiba Mlangoni Kwako ni huduma inayozingatia familia, Wafanyabiashara na Wajasiriamali ambapo mpango mpango huu unapunguza gharama za mawasiliano kwa asilimia kubwa
‘’Huduma hii ya kisasa ya TTCL inaleta suluhisho la mawasiliano bora, na unafuu wa gharama kwa jamii. Kwa sasa shirika linatekeleza ujenzi wa miundo mbinu ya mawasiliano ili kuwawezesha watanzania kupata fursa ya biashara biashara zao kimtandao, kujiunga bila kikwazo, pamoja na huduma mbalimbali za kidigitali za kidigitali,’’alisema Moshi.
Alieleza kuwa huduma hiyo imelengwa nchi nzima lakini wameanza na mkoa wa Dar es Salaam ambapo wanaendelea na usambazaji wa huduma hiyo Kimara,Kawe,Magomeni,Kigamboni na Mbezi.
‘’Tumejipanga vyema kuhakikisha huduma bora za uhakikia na zenye ubora wa kimataifa zinawafikia wateja wetu wote ndani nan je ya Tanzania kupitia uwekezaji endelevu miundombinu ya kisasa na teknolojia na za kisasa za mawasiliano,’’alisema.
Alisema shirika hilo linaendelea kuetekeleza mpango wa upanuzi wa miundombinu ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kueneza mkongo wa taifa wa mawasiliano hadi kufikia wilaya zote za Tanzania.
Alieleza kuwa kilele cha maadhimisho ya wiki hiyo kitakuwa Octoba 10, mwaka huu.Huku yakiwa sambamba na kaulimbiu isemayo’Inawezekana’ ambayo inawapa nguvu ya kuamini kwamba hakuna lisilowezekana wakiamua,wakibuni na wakishirikiana.
‘’Kaulimbiu hii itakuwa dira yetu ya kila siku katika utekelezaji wa majukumu ya shirika katika kutoa huduma kwa wateja,tutakauwa wabunifu,wenye bidi na watumishi wenye maono yanayolenga matokeo na kila mmoja wetu atakuwa sehemu ya suluhisho la kukamilisha huduma anayohiitaji mwananchi,’’alisema
Aliongeza kuwa katika wiki hiyo wamejipanga kuhakikisha miundombinu yao inaboresha maisha ya Watanzania kwa kuwapatia huduma bunifu na zenye ubora wa kimataifa na kuweka ukaribu kwa wateja wao.