Bodaboda wakumbushwa kuvaa kofia ngumu

NJOMBE: WAENDESHA bodaboda wa Kijiwe cha Kanisa Katoliki Romani mkoani Njombe, wametakiwa kuvaa kofia ngumu (helmet) wao pamoja na abiria wakati wakiwa barabarani ili kuzingatia usalama wao.

Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Njombe, Sajent Petro Philomoni, ambapo pia amewaasa kuacha tabia ya kujiingiza katika uhalifu kwa kuwaibia abiria au kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili kama vile ubakaji au ulawiti.

SOMA ZAIDI: Polisi waonywa kukamata bodaboda kwa fimbo

Advertisement

Sambamba na hilo, amewataka kuzingatia Sheria na kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima.

Aidha elimu hii imeendelea kutolewa mkoani Njombe kwa madereva wa vyombo vya moto ili kuwakumbusha sheria mbalimbali usalama barabarani

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *