Dk Chana atua Singida kutatua kero wanyamapori

INGIDA: WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana amewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida leo Oktoba 28,2024 kwa ajili ya kupatia ufumbuzi changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo.

Chana amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson ambapo pamoja na mambo mengine amepokea taarifa kuhusu hali ya udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu mkoani Singida.

Advertisement

SOMA: Dk Chana ahamasisha uwekezaji mazao ya misitu

Akizungumza katika kikao cha awalI, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ametoa maelezo kuhusu tukio la tembo lililotokea katika eneo la kambi ya mkaa wilayani Ikungi Oktoba 26,2024 ambalo lilisababisha taharuki kwa wananchi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)