LONDON: MANCHESTER United inasafiri kutoka Jiji la Manchester kuelekea Fulham Jiji la London kwenda kuikabili timu ya Fulham mchezo wa Ligi Kuu England utakaopigwa uwanja wa Craven Cottage leo saa 4 usiku.
Kwenye msimamo wa ligi hiyo, United inashika nafasi ya 13 wakiwa na pointi 26, wakati wapinzani wao wakiwa nafasi ya 10 pointi 33.
United wameshinda mchezo mmoja katika mitano ya mwisho, huku Fulham wakishinda miwili katika mitano.
Michezo mingine itakayopigwa leo, Spurs watakuwa nyumbani kuwakaribisha Leicester City, Crystal Palace dhidi ya Brentford na Aston Villa dhidi ya West Ham United uwanja wa Villa Park.