Gamondi asisitiza matumizi ya nafasi
KOCHAwa Yanga, Miguel Gamondi amesema wamejipnga kuhakikisha wachezaji wa timu hiyo wanatumia kwa usahihi nafasi watakazotengeneza katika mchezo wa marudiano kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE.
Mchezo huo utachezwa kesho uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar saa 2:30 usiku.
“Mechi iliyopita kweli tulikosa nafasi nyingi. Lakini kama kocha kukosa nafasi hutokea, muhimu ni kuwa na timu yenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi. Ukweli ni kwamba lazima kesho tutumie nafasi tunazopata,” amesema Gamondi.
“Mechi iliyopita kweli tulikosa nafasi nyingi. Lakini kama kocha kukosa nafasi hutokea, muhimu ni kuwa na timu yenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi. Ukweli ni kwamba lazima kesho tutumie nafasi tunazopata. Sitaki kuwapa wachezaji wangu presha kisa tulikosa nafasi nyingi,… pic.twitter.com/opn20685hS
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) September 20, 2024
“Najua watacheza kwa utulivu lakini muhimu ni kuhakikisha tunatumia nafasi tunazopata,” ameongeza Miguel Gamondi.