UGANDA: SERIKALI ya Uganda imetangaza kuwa idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola imefikia tisa kutoka watu watatu tangu ilipobaini ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo imesema wagonjwa 7 kati ya 9 wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali moja iliyopo mjini Kampala na mgonjwa mwingine amelazwa katika hospitali ya mji wa mashariki wa Mbale karibu na mpaka na Kenya.
Mtu mmoja ndiye amekufa tangu ugonjwa huo ulipozuka kulingana na wizara ya afya, wagonjwa wote wanane wako kwenye hali nzuri, na watu 265 waliowahi kukutana na wagonjwa hao wamewekwa karantini.
Hivi sasa Uganda inatoa chanjo ya majaribio dhidi ya kirusi cha Ebola kilichoanzia nchini Sudan.Chanjo ya Ebola iliidhinishwa kutumika an Shirika la Afya Duniani –WHO , mwezi uliopita.