Kamati Afcon 2027 yaridhia uundaji kamati ndogo
DAR ES SALAAM: KAMATI ya Taifa ya Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 imekutana kupitia na kuridhia mapendekezo ya uundwaji wa kamati ndogo pamoja na Sekretarieti ya Kamati hiyo.
SOMA: ‘Tujiandae kwa fursa AFCON 2027’
Kamati hiyo inayoongozwa na m handisi Leodgar Tenga imepitisha kamati hizo ambazo ni Kamati ya Usimamizi wa Miundombinu, Mawasiliano, Fedha, Tiba na “Doping” ,Uendeshaji wa Matukio, Ulinzi na Usalama, (Sheria, Matangazo, Masoko na Biashara), Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari ,Kamati ya Uidhinishaji na watoa huduma.
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.