Kocha Azam FC alia umbali Kigoma
KOCHA wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema kuwa muda mfupi tangu kumaliza mechi na Simba umbali mrefu kutoka Zanzibar hadi Kigoma umemnyima nafasi nzuri ya mapumziko kwa wachezaji kujiandaa kikamilifu dhidi ya ya Mashujaa unaotarajia kufanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Septemba 29.
Kocha huyo raia wa Morocco amesema hayo mkoani Kigoma kuelekea mchezo huo utakaopigwa jumapili katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma na kubainisha kuwa wachezaji wake walitumia nguvu kubwa kwenye mchezo na Simba hivyo walihitaji kupumzika kabla ya kusafiri umbali mrefu kuikabilia mashujaa.
SOMA: Azam FC yapigwa faini Sh milioni 1
Pamoja na hilo kocha huyo amesema kuwa hawatakubali kupoteza tena mechi na Mashujaa baada ya kudondosha pointi tatu kwa Simba kwenye mchezo uliopita.
Mchezaji wa timu ya Azam Nassoro Saadun kwa niaba ya wachezaji wa timu hiyo amesema kuwa wako tayari
kupambana kuhakikisha wanaondoka na point tatu dhidi ya Mashujaa na kwamba wachezaji wana ari kubwa ya kushinda mchezo huo.
SOMA: Daktari wa Azam FC afariki dunia