Makamu wa Pili wa Rais SMZ ahimiza mazoezi

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla ametoa rai kwa wananchi kuwa na mpangilio mzuri wa lishe na kufanya mazoezi ili kupunguza hatari ya kupata maradhi yasiyokuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na magonjwa mengineyo .

Kiongozi huyo ametoa rai hiyo leo Septemba 6, wakati akifungua mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) uwanja wa Jamhuri Morogoro.

“Maradhi haya kwa sasa yamechukua nafasi kubwa ya kuathiri afya ya wananchi walio wengi hapa nchini mwetu kutokana na kutokufanya mazoezi na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa lishe bora,“amesema Abdulla.

Alisema kuwa michezo ni furaha ni afya na ni utalii na kwamba ni chachu ya mafanikio ya mtu mmoja mmoja , taasisi na taifa kwa ujumla, kwani inajenga afya ya akili, mwili, nidhamu na si tu kwa mwanajeshi bali hata kwa mwananchi wa kawaida.

SOMA: Michezo ya majeshi kuanza leo

Hivyo alisema kwa upande wa serikali zote mbili kwa kutambua hilo zinaendelea kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na kushiriki katika michezo pamoja na kula vyakula vya asili ili kupunguza ana kuzuia madhara yatokanayo na ukosefu wa mpangilio mzuri wa chakula na kutokufanya mazoezi.

Kwa upande wa michezo hiyo ya majeshi, alisema kufanyika kwa michezo hiyo ni faraja kwa nchi yetu kwani itasaidia kunyanyua viwango vya michezo.

SOMA: Kombe la Mkuu wa Majeshi Julai 20

“Sote tunaelewa wawakilishi wetu wa kitaifa na kimataifa huwa wanatoka katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama nah ii inajidhihilisha watati jeshi letu ikiweka rekondi ya mnamo mwaka 1974 waliposhinda mbio ya mita 1,500,“ alisema.

Pia alisema mara kadhaa michezo imekuwa kama nyenzo ya kupambana na uharifu na dawa za kulevya kuwasajihisha vijana kujiunga katika michezo ili wazijuhusishe katika vigenge na kuwaepusha kushiriki katika vitendo viovu ikiwamo ubakaji , wizi na ujambazi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia alitoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuedelea kuimalisha timu za majeshi na kuona uwezekano wa kuwaandikisha wanamichezo raia wenye vipaji vya michezo.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza azma ya kauli mbiu ya michezo ni ajira lakini itaendeleza michezo hapa nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button