Mikakati kudhibiti utoroshaji wa madini ilete tija kwa taifa

WATAALAMU kutoka taasisi mbalimbali za serikali wamefanya kikao cha kujadili mikakati ya kudhibiti utoroshaji wa madini nchini, chini ya uongozi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo.

Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, imeelezwa kwamba ni wajibu wa kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika kulinda rasilimali za taifa, hasa madini, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Hatua hii ya serikali ni njema na inapaswa iungwe mkono kwa dhati kwa kuhakikisha inaandaliwa mikakati madhubuti inayo- tekelezeka kwa lengo la kuleta tija nchini.

Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania imejaliwa utajiri mkubwa wa madini kama vile dhahabu, almasi, tanzanite, chuma, nikel na gesi asilia. Utoroshaji wa madini unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu umekuwa ukiisababishia serikali hasara kubwa ya mapato.

Kama alivyosema Mbibo, utoroshaji wa madini ni tishio kwa uchumi na usalama wa taifa letu, hivyo lazima kuwepo ushiriki- ano wa dhati katika kudhibiti mianya yote inayochangia vitendo hivi.

Hivyo, ni muafaka kwa serikali kupitia wataalamu wake kuku- tana na kuunganisha nguvu kwa lengo la kupata njia madhubuti za kupunguza, kama si kuondokana na tatizo hili moja kwa moja.

Imeelezwa kwamba, wadau wamekubaliana kuweka mikakati ya haraka ya utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa, ikiwa ni pamoja na kuandaa mpangokazi wa pamoja utakaohakikisha udhibiti wa utoroshaji wa madini unafanyika kwa ufanisi na kwa muda mrefu.

Tunapongeza hatua hizi tukisisitiza kwamba mikakati hiyo iwe ya kumfanya kila Mtanzania kuona wajibu wa kushiriki kulinda rasilimali hizi kwa manufaa ya wote, badala ya kuachwa mikononi mwa serikali na watendaji wake pekee.

Kila mwananchi anapaswa kuwa mlinzi wa uchumi wa taifa lake kwa kuwafichua watoroshaji wa madini, kutoa taarifa sahihi kwa mamlaka husika na kuepuka kushiriki biashara haramu. Hizi ni miongoni mwa njia bora za kuonesha uzalendo wa kweli unao- jengwa juu ya uadilifu, uwajibikaji na upendo kwa taifa.

Matarajio yetu ni kuona elimu endelevu ikitolewa kwa wa- nanchi, ili waelewe kwamba kulinda madini ni sawa na kulinda mustakabali wa maendeleo yao.

Aidha, mikakati ijikite katika msingi wa uadilifu na uwajibikaji, sambamba na serikali kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti wa teknolojia za kisasa katika migodi, mipaka na bandari ili kufua- tilia kwa ufanisi mienendo ya madini.

Kadhalika, ni muhimu kuwa na watumishi wa umma waami- nifu, wenye weledi na uzalendo wa kweli. Vinginevyo, mikakati bora haina maana kama watendaji wake ni wala rushwa au wasio waadilifu.

Tunaipongeza serikali kwa kuendeleza ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na sekta binafsi katika kulinda madini, tukiamini suala hili ni endelevu katika kudhibiti utoroshaji wa madini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button