Mwenyekiti mstaafu IEBC afariki dunia

Wafula Chebukati.

KENYA: ALIYEKUWA, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, Wafula Chebukati, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Taarifa hiyo, imethibitishwa na mtoto wake Chebukati, Emmanuel ambapo amesema baba yake amefariki akiwa katika hospitali moja iliyopo jijini Nairobi nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu.

Amesema, Chebukati ameugua kwa takriban wiki moja na alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kabla ya kufariki.

Advertisement

SOMA ZAIDI: Mwenyekiti wa Bodi JKCI afariki dunia

Chebukati alihudumu kama Mwenyekiti wa IEBC kuanzia Januari 2017 hadi Januari 17, 2023, akisimamia chaguzi kuu za Kenya za mwaka 2017 na 2022.

Kwa upande wake Rais wa Kenya, William Ruto, amesema “Nimepokea kwa huzuni kubwa habari za kifo cha Mwenyekiti wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati. Kifo chake ni pigo kubwa kwa taifa letu. Mawazo yetu na sala zetu ziko pamoja na familia yake na marafiki katika kipindi hiki kigumu. Apumzike kwa amani,”

Chebukati atakumbukwa kwa kutangaza Rais Ruto kama mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2022, uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali na baadaye kusababisha mgogoro ndani ya Tume. Chebukati alitangaza kuwa Ruto alishinda kwa asilimia 50.49 ya kura, dhidi ya Raila Odinga wa Azimio aliepata asilimia 48.5.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *