PICHA| Safari ya mwisho ya bosi wa Tanesco

BUNDA — Mamia ya waombolezaji wamejitokeza leo Aprili 16, 2025, katika mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga yaliyopangwa kufanyika nyumbani kwake, Migungani, Bunda mkoani Mara.
Shughuli hizo zimehudhuriwa na viongozi wa serikali wakiongozwa na Naibu Waziri Mkuu Dk Doto Biteko, watendaji wa sekta ya nishati, familia na marafiki waliokuja kutoa heshima za mwisho kwa mmoja wa wahandisi waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya umeme nchini.
Wakati wa mazishi hayo, viongozi mbalimbali walitoa salamu za rambirambi wakimtaja Mhandisi Nyamo-Hanga kama “kiongozi aliyekuwa na maono na mtumishi wa umma mwenye uzalendo wa dhati kwa taifa lake.”
Kwa mujibu wa familia, Mhandisi Gissima atakumbukwa kwa weledi wake, uadilifu na jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa umeme vijijini na mijini kote nchini.
Mazishi hayo yanafanyika kwa heshima zote za kitaifa, yakitamatishwa na sala maalum ya kuombea marehemu apumzike kwa amani.