Rahisisheni kazi ya Wanahabari- Majaliwa

DODOMA: WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wa Serikali waondoe ukiritimba kwenye suala la upatikanaji wa habari ili kuwawezesha wanahabari kupata taarifa sahihi na kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Ametoa wito huo leo Mei,3,2024 wakati akizungumza na wanahabari na wadau wengine kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Isome pia https://habarileo.co.tz/majaliwa-acheni-kukopakopa-wanahabari/

Aidha,Majaliwa amewataka wakuu wa taasisi waweke mazingira mazuri kwa waandishi wa habari ili kuwawezesha kuzingatia weledi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa ngazi zote za jamii.

 

“Viongozi na Watendaji wa Serikali na Mashirika zingatieni Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa ya Mwaka 2016 na ondoeni ukiritimba katika suala la upatikanaji wa habari ili wanahabari wawezeshwe kupata taarifa sahihi na wafanye kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu,” amesema Waziri Mkuu.

Isome pia https://habarileo.co.tz/wanahabari-tumieni-vizuri-kalamu-zenu/

Pia,amevitaka vyombo vya habari viunde madawati maalum yatakayoratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

“Madawati hayo yatafute fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango wa mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu kuandika kitaalamu masuala ya mabadiliko ya tabianchi na madhara yake kwa jamii na Taifa. Suala hili likamilike ili katika maadhimisho ya siku hii mwakani, iwepo taarifa ya utekelezaji,” amesema Majaliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button