Wanachama CUF waitwa ACT
KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amewakaribisha wanachama na wafauasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kujiunga na chama chao akiamini kwa sasa chama hicho kinakuwa kwa kasi.
Akizungumza Septemba 15 katika ziara yake kata ya Ruaruke, jimbo la Kibiti, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Ado Shaibu amesema ACT ndio jahazi sahihi kwa wafuasi wa CUF jimboni hapo hivyo ni wakati sahihi kuendeleza mapambano.
“Tutawapokea wote kwa mikono miwili na kwa pamoja tutaendeleza sera zilezile za haki sawa kwa wote ili kujenga ‘taifa la wote kwa maslahi ya wote’ na ‘Zanzibar Mpya, Zanzibar Moja Mamlaka Kamili,” Ado amesema.
SOMA: ACT Wazalendo kusherehekea utumishi wa Juma Duni
Kiongozi huyo amesema baada ya Maalim Seif Sharif Hamad kujiunga na ACT Wazalendo wafuasi wengi wa CUF walimfuata na kwamba hatua hiyo sio tu ilikipa nguvu chama hicho, lakini pia ilibadili ramani ya kisiasa nchini.
SOMA: ACT Wazalendo waivuruga Chadema Lindi
Leo nimekutana na viongozi wa uliokuwa Mkoa wa Pwani ambao Halmashauri Kuu Taifa ya ACT Wazalendo imeugawanya kwenye Mikoa miwili ya Kichama ya Pwani na Mwambao.
Kwenye kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wa iliyokuwa Kamati ya Uongozi ya Pwani na Wenyeviti na Makatibu wa… pic.twitter.com/LvYdcT5fwP
— Ado Shaibu (@AdoShaibu) September 15, 2024