ANGOLA: WATU 108 wamekufa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu tangu ugonjwa huo ulipoanza Januari mwaka huu nchini Angola.
Taifa hilo la Afrika lenye utajiri mkubwa wa rasilimali limekuwa likikabiliwa na umaskini na hali duni ya usafi wa mazingira licha ya utajiri wake wa mafuta
Soma zaidi: https://habarileo.co.tz/mbogamboga-matunda-chanzo-cha-kipindupindu/
Taarifa hiyo imetolewa na Wizara ya Afya nchini humo, ambapo imesema Mji Mkuu wa Luanda ni miongoni mwa miji iliyoathirika ambapo watu 48 wamefariki dunia na watu 45 kutoka jimbo jirani la Bengo.
Soma zaidi: https://habarileo.co.tz/vifaa-tiba-kukabiliana-na-kipindupindu-kanda-ya-ziwa/
Shirika la Afya Duniani lilisema mwaka jana kuwa vifo vitokanavyo na kipindupindu duniani kwa mwaka 2023 viliongezeka kwa asilimia 71 ikilinganishwa na mwaka uliopita.