‘Yoro hana makubaliano ya maandishi Man United’

TETESI za usajili zinasema Leny Yoro hana makubaliano ya maandishi na ‘Mashetani Wekundi’ Manchester United jambo ambalo litamruhusu kujiunga na Real Madrid wakati ujao kwa ada ya pauni milioni 42.5. (Defensa Central – Spain)

Liverpool inataka kumsajili beki wa Bayer Leverkusen Piero Hincapie, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 42.5 kabla ya Atletico Madrid, Bayern Munich, Man Utd, na Tottenham Hotspur. (Diaro Expreso – Uhispania)

Beki wa Bayer Leverkusen, Piero Hincapie

Pia Mohamed Simakan wa RB Leipzig ambaye yuko tayari kuondoka klabu hiyo ya Bundesliga pia yupo katika rada za Liverpool.(Sky Sports Germany)

SOMA: Man United yapanga kumuuza Sancho kwa vigogo

Man City imekubali kumuuza beki wa pembeni, Joao Cancelo kwenda klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kwa zaidi ya pauni milioni 29.8. (City Report)

Barcelona pia inamwinda Cancelo lakini klabu hiyo ya La Liga pia inafikiria uwezekano wa Marc Pubill wa Almeria awe mbadala. (SPORT – Spain)

Habari Zifananazo

Back to top button